Playing via Spotify Playing via YouTube
Skip to YouTube video

Loading player…

Scrobble from Spotify?

Connect your Spotify account to your Last.fm account and scrobble everything you listen to, from any Spotify app on any device or platform.

Connect to Spotify

Dismiss

A new version of Last.fm is available, to keep everything running smoothly, please reload the site.

Siku Moja - Lyrics

Waimbaji wengi wanajiamini
Lakini hawaaminiki
Ukitaka kujua kisa hichi
Fuatilia wimbo huu kwa makini

Siku moja nikiwa Kyela
Nawe Abura na Pastor Kasunga
Kwa huruma Kasunga kaniambia
Abiudi Mungu akusaidie
Umwombe Mungu Mchungaji Abiudi
Umeingia kwenye huduma hii
Huduma hii ya uimbaji
Ni ya watu wasiohudumu
Tena Kasunga sishangai mbona
Waimbaji wengi wakirudi nyuma
Hata shetani wa kwanza kuimba
Naye pia alirudi nyuma
Sasa nifanyeje

Yesu ninakuja kwako
Msalabani najinyenyekeza
(Nishike) Nishike nami nikushike
Ukiniacha nitaaibika
(Ninaomba) Kiburi kiwe mbali nami
Huo uzinzi usitajwe kwangu
(Usiruhusu) Usiruhusu anguko lije kwangu
Nikasinyaa kwa mawazo mengi
(Nitakimbilia) Nitakimbilia wapi mimi
(Dunia) Dunia n'taiona ndogo
(Mke wangu) Mke wangu n'tamfariji vipi
(Kanisa lako) Kanisa lako n'taliambia nini

Wimbo huu
Unaweza leo usiuelewe
Mchungaji, mwimbaji
Lakini siku ukitenda dhambi
Wimbo huu utaukumbuka
Lakini lengo langu
Si kuona unatenda dhambi
Bali unaendelea mbele
Ni aibu mno
Mtumishi kutenda dhambi

Nikaendelea kutafakari
Eti siku ije, kweli Abiudi nitende dhambi
Mungu niepushe
Siku ya kutisha na ya giza zito
Hapo Mungu atakaponiacha
Nitaendelea kujitutumua
Huku moyoni nimekwisha oza
Ndipo maaskofu watakapokuja
Kunifukuza mimi hekaluni
Nitaondoka huku nimeloa
Wal'onipenda wataomboleza
Mke wangu atazirai
Was'onipenda watafurahia
Nimejitwika na jina la Mungu
Madhabahu yake nimepaka tope
Wanadamu n'tawaonea aibu
Nimejivua nguo hadharani
Sasa nifanyeje

Yesu ninakuja kwako
Msalabani najinyenyekeza
(Nishike) Nishike nami nikushike
Ukiniacha nitaaibika
(Ninaomba) Kiburi kiwe mbali nami
(Uzinzi) Huo uzinzi usitajwe kwangu
(Usiruhusu) Usiruhusu anguko lije kwangu
(Nitakonda) Nikasinyaa kwa mawazo mengi
(Nitakimbilia) Nitakimbilia wapi mimi
(Dunia) Dunia n'taiona ndogo
(Mke wangu) Mke wangu n'tamfariji vipi
(Kanisa lako) Kanisa lako n'taliambia nini

Mtumishi Kasunga alinionea huruma
Akasema umwombe Mungu Mchungaji Abiudi
Umeingia katika huduma ya watu wasiohudumu
Ni kweli, waimbaji wengi
Wamekuwa na tabia ya kuangukaanguka na kurudi nyuma
Lakini ninachosikitika
Si waimbaji tu, bali hata na wachungaji sasa
Wamekuwa wanarudi nyuma
Lakini lengo langu
Si kuona ya kwamba tunarudi nyuma
Bali tunaendelea mbele
Na tunailinda imani
Pia, nirudi kwako mheshimiwa Kasunga
Nawe pia umwombe Mungu usirudi nyuma
Kwa sababu Bibilia inasema hivi
Hatukufika, bali tunakaza mwendo
Ili kuifikia meli ya thawabu
Mungu akubariki, mtumishi mwenzangu
Nakutakia huduma njema
Uendelee mbele, tumwombe Mungu
Nami pia nimwombe Mungu
Kwa sababu ni aibu mno mtumishi wa Mungu kurudi nyuma
Mungu atusaidie, Mungu akusaidie

Don't want to see ads? Subscribe now

API Calls