Playing via Spotify Playing via YouTube
Skip to YouTube video

Loading player…

Scrobble from Spotify?

Connect your Spotify account to your Last.fm account and scrobble everything you listen to, from any Spotify app on any device or platform.

Connect to Spotify

Dismiss

A new version of Last.fm is available, to keep everything running smoothly, please reload the site.

Boss - Lyrics

Homa kali imenichachamaa mwilini
watoto wiki ya pili wamefukuzwa ada shuleni
na mtaani sina amani nimeandamwa na madeni
mama watoto wahi kazini kwangu upate taarifa
kama kuna msaada wowote bosi anaweza kupa aaaaaah
Alfajiri iliofuata Mama akajidamka,
Tukaagana vizuri, kazini kwangu akaibuka
kufika pale bila ya kuipoteza mida
akaingia ofisini na kuanza kueleza shida
okay okay. Bosi akamkubalia
na fedha akampatia, Kumbe tayari alikuwa ameshamzimia
ili kumkoleza, fedha akamuongeza
katika maongezi maongezi bossi akamtongoza
Mama akiangalia hali aliyoiacha nyumbani,
Ni dhiki kubwa ambayo kwakweli hakuitamani
Na kama unavyoelewa mapenzi ya sikuhizi,
Alisha ahidiwa atagharamiwa yote matumizi
Ikibidi akubali tena bila kipingamizi
Baada ya kupita kipindi mapenzi yakaanza
shamiri, Huku kabwela mimi sina hile wala hili
Bosi akaanza kunipa safari nyingi za kikazi,
ili nikiondoka apate nafasi ya kumwaga radhi
Hadi kufika hapo mi sikuelewa, kama kuna picha ninayochezewa.
Wafanyakazi wenzangu wakaja nishtua,
kwamba sikuhizi wife wako bosi anamchukua.
Kwakuwa nilimuamini sana wife nilibisha,
lakini baada ya kuchunguza nikaja hakikisha.
Nikamwambia mama watoto ila akakataa,
nikimueleza bwana mkubwa itakuwa kizaa zaa, Itakuwa kizaa zaa.
Wanasema sikubali bora niangamie, wengine wanasema heri nivumilie
kwengine wapi ntapata ajira nambie,
Na elimu yangu ndo vile mwenzangu na mie
Watoto wataishi kwenye yapi mazingira,
nikimwambia bwana mkubwa ntaikosa ajira
Taswira yangu ilipoanza kukosa mwangaza,
nafsi ikaanza dhohofika kwaajili ya kuwaza
Hata muda mrefu hauchukua, nikazidi kuchanganyikiwa nilivyogundua
Nilivyogundua kwamba, Laazizi wangu.
wa waridi la maisha amebeba mimba kwenye mazingira yalionitatanisha
jiujezi mbwiga aliekosa wazazi, nikashindwa kula wala kupata usingizi
nikawa nakesha, nikimuomba manani anijalie muelekeo
huku nikivuta subra kusubiri matokeo,
Ila sikuamini yangu macho, ilipofika kipindi ambacho
wife wangu alipojifungua ujauzito,
kuzaliwa mtoto kafanana na yule kizito
Akili ikanituma nichukue panga au rungu,
ili niende kumdhuru yule mtoto kwa uchungu.
Nahisi malaika wakapooza jazba zangu,
na kunikumbusha kuwa kile ni kiumbe cha mungu
Baada ya kupita siku tatu wakaja wafanyakazi
wenzangu, kunipa pongezi wakiwa na yule bosi wangu
Machungu yalinijaa moyoni, lakini nilishindwa nifanye nini.
Nikimuharibia bosi ntafukuzwa kazini.
Wadhifa wake wafanya apate ninyanyasa,
nami kuishi hivyo nafsi yangu inakataa
Nachohofia endapo kazi nitaikosa,
watoto wataishi vipi naomba ushauri wa kufuata
mwenzenu mimi, mwenzenu mimi
Wanasema sikubali bora niangamie, wengine wanasema heri nivumilie
kwengine wapi ntapata ajira nambie,
Na elimu yangu ndo vile mwenzangu na mie
Watoto wataishi kwenye yapi mazingira,
nikimwambia bwana mkubwa ntaikosa ajira
Wanasema sikubali bora niangamie, wengine wanasema heri nivumilie
kwengine wapi ntapata ajira nambie,
Na elimu yangu ndo vile mwenzangu na mie
Watoto wataishi kwenye yapi mazingira,
nikimwambia bwana mkubwa ntaikosa ajira
Juma nature:
we feruzi muharibie, muharibie uyo, mkate kidevu
boss mkurugenzi kitambi meneja
usione tumekonda ukadhania mateja
sasa ndo umemfanya nini mfanyakazi mwenzetu?
Si umemchukulia mkewe ndoman analalamika.
Au kuna jingine feruzi hataki kuwajibika
sikiliza mwanangu feruzi, hapa hatoki mtu.!
ukisema umuache utakuwa umeidhulumu nafsi,
yani najiskia vibaya kwanini huyu bosi hafi, Ananiudhi.
Feruzi mharibie, mbona unasita sita?
Feruzi mkate kidevu mzee, Au unamuogopa?
Naweza, Hivyo naweza, ninachohofia familia kuiteketeza
Nyumba ninayokaa ni mali ya shirika,
nitaenda ishi wapi bosi akikasirika?
Ukoo mzima mimi unanitegemea, na mimi kazini pale ndo nilipoegemea.
Kutokana na unyama bosi alionitendea,
wengine wanashauri hata kwa mganga ningemwendea
Feruzi basi, hebu tuliza nafsi, pole sana kwa mkasa wa bosi.
tumuombe mungu aondoe mikosi, achana na visasi, (utakuja jijutia)
Yani ishakuwa nuksi, ndoa ina ibilisi
basi, chana karatasi
talaka tatu sio dawa ya mkosi
we unatoa chansi ya uu mikasi
Dhiki, ibilisi na vichocheo vya
bosi, mkeo vilimshawishi aonekane ni muasi
Wewe ubaki na kazi, uroda alipewa bosi
Ingawa kwa nia njema, ili wanao wasile nyasi
vumilia ni mtihani umekujia, mshinde shetani hata vitabu vinatuambia
Mungu anasamehe, na wewe samehe pia.
Kama amekiri kosa, mkanye asije rudia.
ooooh oooh hapana, hapana, hapana,
Hivyo ndo utaharibu kabisa, hivyo ndo utaharibu kabisa,
Nishaishi vipi kama mtumwa anaekosa
uhuru, Akati mie hali hio kibinafsi inanidhuru.
Kitu kinachoniongeza machungu
kubambikiwa mtoto ambae si damu yangu...
eeeh mola nisaidie,
nipo kwenye janga la utata, nipo kwenye janga la utata
Wanasema sikubali bora niangamie, wengine wanasema heri nivumilie
kwengine wapi ntapata ajira nambie,
Na elimu yangu ndo vile mwenzangu na mie
Watoto wataishi kwenye yapi mazingira,
nikimwambia bwana mkubwa ntaikosa ajira
Wanasema sikubali bora niangamie, wengine wanasema heri nivumilie
kwengine wapi ntapata ajira nambie,
Na elimu yangu ndo vile mwenzangu na mie
Watoto wataishi kwenye yapi mazingira,
nikimwambia bwana mkubwa ntaikosa ajira

Don't want to see ads? Subscribe now

API Calls